Robo Mwezi
Watumishi wa Campoverde
Imetafsiriwa na Kennedy Langat
Hakimiliki © 2019 M.G. Gullo – M. Longo
Picha ya jalada na michoro iliundwa na kuahiririwa na Massimo Longo
Haki zote zimehifadhiwa
ISBN
ISBN-13:
JEDWALI YA YALIYOMO
Sura ya Kwanza Anaepuka nikijaribu kumkumbatia... Sura ya Kwanza Anaepuka nikijaribu kumkumbatia... |
|
Sura ya Pili Mnong'ono wa baridi ulikuwa ukimsumbua Sura ya Pili Mnong'ono wa baridi ulikuwa ukimsumbua |
|
Sura ya Tatu Aligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kicheko Sura ya Tatu Aligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kicheko Sura ya Tatu Aligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kicheko |
|
Sura ya nne Sauti ilikuwa ikinong'oneza masikioni mwake maneno kwa lugha isiyojulikana Sura ya nne Sauti ilikuwa ikinong'oneza masikioni mwake maneno kwa lugha isiyojulikana |
|
Sura ya Tano Anakabiliwa na kitu cha kuogofya Sura ya Tano Anakabiliwa na kitu cha kuogofya |
|
Sura ya Sita Hakuweza kutoa matamshi hayo kutoka kwa kichwa chake Sura ya Sita Hakuweza kutoa matamshi hayo kutoka kwa kichwa chake |
|
Sura ya Saba Wahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutuliza Sura ya Saba Wahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutuliza Sura ya Saba Wahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutuliza |
|
Sura ya Nane Tafakari ya picha hiyo mbaya Sura ya Nane Tafakari ya picha hiyo mbaya |
|
Sura ya Tisa Ngazi isiyo na mwisho Sura ya Tisa Ngazi isiyo na mwisho |
|
Sura ya Kumi Alihisi kama angeweza kutoboa mbingu kwa mikono yake wazi Sura ya Kumi Alihisi kama angeweza kutoboa mbingu kwa mikono yake wazi |
|
Sura ya Kumi na Moja Wazo hili liliendelea kuitesa royo yake Sura ya Kumi na Moja Wazo hili liliendelea kuitesa royo yake |
|
Sura ya Kumi na Mbili Ilimkumbusha kinywaji cha vitunguu vya kiberiti Sura ya Kumi na Mbili Ilimkumbusha kinywaji cha vitunguu vya kiberiti |
|
Sura ya Kumi na Tatu Alishuka kutoka angani akikokota mawingu yake meusi Sura ya Kumi na Tatu Alishuka kutoka angani akikokota mawingu yake meusi |
|
Sura ya Kumi na Nne Alishuka chini ya wingu Sura ya Kumi na Nne Alishuka chini ya wingu |
|
Sura ya Kumi na Tano Kama kwamba alimezwa na Dunia Sura ya Kumi na Tano Kama kwamba alimezwa na Dunia |
|
Sura ya Kumi na Sita Ghafula kelele za ajabu zilisikika kama za kigugumizi cha kina Sura ya Kumi na Sita Ghafula kelele za ajabu zilisikika kama za kigugumizi cha kina |
|
Sura ya Kumi na Saba Alikuwa akitembea vizuri wakati alipovuka kizingiti Sura ya Kumi na Saba Alikuwa akitembea vizuri wakati alipovuka kizingiti |
|
Sura ya Kumi na Nane Makucha yaliingia ndani ya ngozi yake Sura ya Kumi na Nane Makucha yaliingia ndani ya ngozi yake |
|
Sura ya Kumi na Tisa Kama kana kwamba ilikuwa Sukari ya barafu kupamba keki ya sifongo ya Victoria Sura ya Kumi na Tisa Kama kana kwamba ilikuwa Sukari ya barafu kupamba keki ya sifongo ya Victoria |
|
Sura ya Ishirini Kila wakati mtoto akiniita kwa jina fulani, ndivyo nitakavyoitwa Sura ya Ishirini Kila wakati mtoto akiniita kwa jina fulani, ndivyo nitakavyoitwa |
|
Dibaji
"Kila kitu kitakuwa sawa, wewe ni mvulana mkubwa sasa....Rudi na ucheze na Watoto wengine. Tutakutana tena, ninakuahidi''
Mtoto alimtazama akitiririkwa na machozi alipoondoka mtu ambaye amekuwa akicheza naye tangu mwanzoni.
Mtoto alikimbia kurejea kwenye vijigari kwenye bustani iliyojuani, ambako alikwenda kucheza na watoto wengine jirani, huku fikra za rafiki ya kimawazo zikififia polepole.
Baada ya kujipenyeza kwenye mahali watoto wengine walikuwa, hatimaye angeweza kupanda kwa kitelezo. Hakupoteza hata muda na alianza kuteleza kwenda chini ya kitelezo, akisukuma kwa bidii kadri awezavyo. Hakuteleza hata hadi mwisho, wakati alipoona msichana mwenye nywele nyeupe akikimbia kutoka kwa mama yake na kuelekea kwenye miguu yake. Hakuweza kupunguza mwendo na alimgonga kwa nguvu.
Msichana huyo mdogo alipoteza mwelekeo na kugonga kichwa chake kwenye ukingo wa kitelezo.
Alijaribu kumfikia mtoto huyo msichana ili kuhakikisha kuwa alikuwa sawa, lakini akasukumwa kando bila huruma na mamaye, ambaye alikuja kumwokoa. Ghafula, kundi la babu na akina mama walikusanyika karibu na msichana huyo maskini.
Alipokuwa akijaribu kutambaa mbali na miguu ya watu wazima, alihisi kwamba alikuwa amezimia. “Mtu mmoja aliita ambulensi!” Huku sauti hiyo ikijitokeza kwa nguvu kwenye maskio yake, alianza kuingiwa na hofu. Alikimbia kuelekea msituni nyuma ya bustani.
Ghafula, kila kitu karibu naye kikawa giza. Upepo baridi ulikuwa umesheheni sauti za kutisha. Mistari asiyoijua ilianza kuchanganyika na mazungumzo ya wazazi kwenye bustani. Zilikuwa zikitoka nyuma ya kundi la miti, ambayo vivuli vyao virefu vilikuwa vinajidhihirisha. Kisha, sauti hiyo ambayo ilikuwa ikijitokeza kutoka pande tofauti ilizidi kuendelea kusikika. Alikuwa akimfikia zaidi na zaidi, hadi alipohisi kuwa ilikuwa ikinong'oneza maskioni mwake:
"Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom…"
Aliweka kichwa chake kwenye mikono yake ili kutuliza sauti hiyo, lakini haikusaidia. Alipiga magoti na akafunga macho yake...
"Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom…"
Sura ya kwanza
Anaepuka nikijaribu kumkumbatia……….
"Elio, Elio, njoo hapa! Nisaidie kuanua mboga kabla ya dharuba kuja, tafadhali."
Elio alikuwa amesimama wima akiwa amevalia viatu vyake vipya na alikuwa akimtazama mamaye, ambaye alikuwa akihangaika katika shughuli zake.
"Elio! Usisimame tu hapo! Chukua hii!" Alimtikisa na kuweka begi iliyojaa mboga kwenye mikono yake. Elio hakuwa na nia ya kufanya kitu kingine. Alipanda ngazi zilizoko nje ya jengo, akageuka na kufungua mlango. Alianza kutazama taa nyekundu ya lifti ambayo mwangaza wake haivumiliki. Kisha, akaacha kusubiri na kupanda ngazi kwenda kwenye nyumba yake gorofani. Aliweka mboga kwenye meza ya jikoni na kwenda moja kwa moja hadi chumba chake cha kulala kusikiza muziki kitandani.
Читать дальше