1 WALIOKATALIWA
Hadithi ya Kuchekesha ya Kisasa ya Familia ya Popo
imeandikwa na
1 Owen Jones
Kutafsiriwa na
1 Kennedy C. Langat
Hakimiliki Owen Jones 14 Agosti, 2021
Haki ya Owen Jones kutambuliwa kama mwandishi wa kazi hii imethibitishwa kulingana na kifungu cha 77 na 78 cha Sheria ya Hakimiliki na Hati miliki ya 1988. Haki ya maadili ya mwandishi imesisitizwa.
Katika kazi hii ya kubuni, wahusika na hafla ni mambo ya mawazo ya mwandishi au hutumiwa kabisa kwa kubuni. Sehemu nyingine zinaweza kuwapo, lakini hafla hizo ni za kubuni.
Imechapishwa na
Huduma za Uchapishaji za Megan
https://meganthemisconception
1 TABARUKU
Kitabu hiki ni kwa heshima ya rafiki zangu Lord David Prosser na Murray Bromley, ambao walinisaidia mimi na familia yangu ya Thai zaidi ya vile watakavyotambua mnamo mwaka 2013.
Asante pia ni kwa SJ Agboola, ambaye ametafsiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiyoruba, kwa kutoa maoni kuhusu maandishi hayo.
Matendo yao mazuri yatalipa kila mtu kwa wema.
Wasiliana nami kwa:
http://twitter.com/lekwilliams
owen@behind-the-smile.org
http://owencerijones.com
Jiunge na jarida letu kwa habari ya ndani
kwenye vitabu na uandishi wa Owen Jones
kwa kuandika barua pepe yako kwa:
http://meganthemisconception.com
1 1 SHIDA ZA BWANA LEE
Bwana Lee, au Mzee Lee, kama alivyojulikana kijijini alikuwa akihisi kiajabu kwa majuma kadhaa, na, kwa sababu jamii ya eneo hilo ilikuwa ndogo sana na iliyotengwa, kila mtu katika maeneo ya karibu alijua pia. Alikuwa akienda kutafuta ushauri kwa daktari wa mtaani, mmoja wa aina ya zamani, sio daktari wa kisasa na alikuwa amemwambia kuwa joto la mwili wake halikuwa sawa, kwa sababu kuna kitu kilikuwa kikiathiri damu yake.
Mwanamke huyo, Mganga wa eneo hilo, ambaye ni shangazi ya Bwana Lee, kwa kweli, bado hakuwa na uhakika kabisa wa sababu hiyo, lakini alikuwa ameahidi kwamba atajua katika saa kama ishirini na nne, ikiwa angeacha sampuli kadhaa ili achunguze na arudi wakati atakapomwita. Mganga alimkabidhi Bwana Lee mkusanyiko mmea wa kuvumwani na jiwe.
Alijua nini cha kufanya, kwa sababu alikuwa ameifanya hapo awali, kwa hivyo akakojoa juu ya mmea wa kuvumwani na akatema mate kwa jiwe baada ya kukohoa kwa kina. Alimrudishia kwa uangalifu asiguse kwa mikono yake asije akaichafua, akaifunga kando kwa vipande vya jani la ndizi kuhifadhi unyevu wao kwa muda mrefu iwezekanavyo.
“Uipatie siku moja ili zioze na ukaushe, kisha nitaangalia vizuri na kuona shida yako ni nini.”
“Asante, Shangazi Da, namaanisha, Mganga Da. Nitasubiri wito wako na nitarudi mara moja utakaponiita. ”
“Subiri hapo, kijana wangu, bado sijamaliza na wewe.”
Da alijisogeza nyuma yake na kuchukua kopo la udongo kutoka kwenye rafu. Aliifungua, akakunywa mara mbili kisha akatema ya mwisho kwa Mzee Lee. Wakati Da alikuwa akisali sala kwa miungu yake, Bwana Lee alikuwa anafikiria kuwa alikuwa amesahau kuhusu ‘utakaso’ - alichukia kutemewa mate na mtu yeyote, lakini haswa wanawake wazee wenye meno yaliyooza.
“Hiyo fukizo la pombe na sala itakusafisha hadi tuweze kutatua shida yako vizuri,” alimhakikishia.
Mganga Da alisimama kama mmea wa Yungiyungi kwenye sakafu ya udongo ya mahali pake pa matibabu, akaweka mkono wake karibu na bega la mpwa wake na kutembea naye nje, akisokota sigara walipokuwa wakienda.
Wakati walipokuwa nje, aliiwasha, akavuta kwa kina na akahisi moshi umejaa kwenye mapafu yake. “Habari ya mke wako na watoto wako wa kupendeza?”
“Ah, wako vizuri, Shangazi Da, lakini nina wasiwasi kidogo kuhusu afya yangu. Nimekuwa nikisikia kizembe kwa muda sasa na sijawahi kuugua katika maisha yangu yote, kama unavyojua. ”
“Hapana, sisi wana-Lee tuna nguvu sana. Baba yako, ndugu yangu mpendwa, angekuwa bado yuko fiti sasa, ikiwa asingekufa na homa. Alikuwa na nguvu kama nyati. Utamrithi, lakini hakuwahi kupigwa risasi. Nadhani ndio iliyokupata, ile risasi ya Yankee. ”
Bwana Lee alikuwa amepitia hii mara mia kadhaa hapo awali, lakini hakuweza kushinda hoja hiyo kwa hiyo aliiitikia kwa kichwa tu, akampa shangazi yake noti hamsini ya Baht na kuondoka kwenda shamba lake, ambalo lilikuwa mita chache tu nje ya kijiji.
Alikuwa anajisikia vizuri tayari, kwa hivyo alitembea kwa mwendo wa furaha kujaribu kuthibitisha kwa kila mtu.
Mzee Lee alimwamini kabisa shangazi yake wa zamani Da, kama kila mtu mwingine katika jamii yao, ambayo ilikuwa kijiji kidogo cha nyumba kama mia tano na mashamba kadhaa. Shangazi yake Da alikuwa amechukua jukumu la kuwa Mganga wa kijijini wakati alikuwa kijana, na hakukuwa na watu ambao wangeweza kumkumbuka yule aliyemtangulia. Hawakuwa wamewahi kuwa na daktari wao aliyehitimu wa chuo kikuu.
Hiyo haimaanishi kwamba wanakijiji hawakuwa na uwezo wa kupata daktari, lakini walikuwa wachache - daktari wa kudumu wa karibu alikuwa ‘mjini’, umbali wa kilomita sabini na tano na hakukuwa na mabasi, teksi au treni katika milima ambako walikuwa wakiishi ulio kwenye kona ya juu kabisa ya kaskazini-mashariki mwa Thailand. Licha ya hayo, madaktari walikuwa wa bei ghali na waliagiza dawa za gharama kubwa, ambazo kila mtu alifikiri walipata asilimia kubwa ya faida. Kulikuwa pia na kliniki katika vijiji vichache vilivyoko mbali, lakini ilikuwa na mwuguzi wakati wote na daktari wa muda ambaye alifanya kazi huko siku moja katika muda wa majuma mawili.
Wanakijiji kama Bwana Lee walidhani kwamba labda hiyo ilikuwa sawa kwa wenyeji matajiri wa jiji, lakini haina maana kwao. Je! Mkulima anawezaje kuacha kazi yake kwa siku nzima na kukodi mtu mwingine aliyena gari kumpeleka kwenda kumtembelea daktari wa jiji? Ikiwa ungepata mtu mwenye gari kijini, ingawa kulikuwa na matrekta machache ya zamani karibu ndani ya kilomita kumi.
Hapana, alifikiria, shangazi yake mzee alikuwa mzuri kwa kila mtu mwengine na alikuwa mzuri kwake na kwa kuongezea, hakuwa amemruhusu mtu yeyote afe ambaye muda wake ulikuwa haujaisha na hakika hakuwa ameua mtu yeyote, kila mtu angeapa kuthibitisha hayo. Kila mtu.
Bwana Lee alijivunia shangazi yake, na hata hivyo, hakukuwa na mganga mbadala kwa maili kadhaa na hakika hakuna mtu aliye na uzoefu kama wake wote - wote…? Kweli, hakuna mtu aliyejua alikuwa na umri gani kweli, hata yeye mwenyewe, lakini labda alikuwa na umri wa miaka tisini.
Bwana Lee alifika uani kwake na mawazo haya akilini. Alitaka kuzungumzia swala hilo na mkewe, kwa sababu ingawa alionekana kwa ulimwengu wa nje kuwa bosi katika familia yake, kama ilivyokuwa kwa kila familia nyingine, hiyo ilikuwa tu oneesho, kwa sababu kwa kweli, kila uamuzi ulifanywa na familia kwa ujumla, au angalau watu wazima wote.
Hii itakuwa siku ya kushangaza, kwa sababu Wana-Lee walikuwa hawajawahi kuwa na “shida” hapo awali na watoto wao wawili, ambao hawakuwa watoto tena, wangeweza kuruhusiwa kutoa maoni yao pia. Historia ilikuwa karibu kutengenezwa na Bwana Lee aliijua vizuri.
“Tope!” aliita, jina lake la upendo kwa mkewe tangu mzaliwa wao wa kwanza hakuweza kusema ‘Mama’. “Tope, upo?”
“Ndio, niko nje nyuma.”
Lee alisubiri kwa muda mfupi ili aingie kutoka chooni, lakini kulikuwa na joto na harufu mbaya ndani ya nyumba, kwa hivyo alirudi kwenye ua wa mbele na kukaa kwenye meza yao kubwa ya familia na paa lake la nyasi ambapo familia nzima ilikula na ilikuwa kawaida kukaa hapo wakati hawana kitu cha kufanya.
Jina halisi la Bi Lee lilikuwa Wan, ingawa mumewe alikuwa akimwita Tope kwa upendo, kwa kuwa mtoto wao mkubwa alikuwa amemwita hivyo na jina hilo lilikuwa limekwama kwa Bwana Lee lakini si kwa watoto. Alitoka kijijini, Baan Noi, kama Lee mwenyewe, lakini familia yake haikujua mahali pengine popote, wakati familia ya Bwana Lee ilitoka Uchina vizazi viwili hapo awali, ingawa mji huo wa nyumbani haukuwa mbali pia.
Alikuwa kawaida kama wanawake wa eneo hilo. Katika siku zake, alikuwa msichana mrembo sana, lakini wasichana hawakupewa nafasi nyingi wakati huo na wala hawakuhimizwa kuwa na tamaa, sio kwamba mambo yalikuwa yamebadilika sana kwa binti yake hata miaka ishirini baadaye. Bi Lee alikuwa ameazimia kutafuta mume akimaliza shule, kwa hivyo wakati Heng Lee aliuliza mkono wake na kuwaonesha wazazi wake pesa za fidia alizokuwa nazo kwenye benki, alikuwa anafikiria kuwa alikuwa mzuri kama mtu mwengine yeyote ambaye angeweza kupata. Wala hakuwa na hamu yoyote ya kutangatanga mbali na rafiki zake kwenye uhusiano na jiji kubwa ili kuongeza upeo wake.
Читать дальше